Mimi Wako Mwenziyo

Nipe nikupe, maneno hayo usemayo,
usinitumie sin’tupe, mimi wako mwenziyo,
sijifananishe kupe, mambo hayo tia moyo,
kwa wakati simo, sijitafutie mwingine.

kwa wakati simo, sijitafutie mwingine,
mapenzi mambo muhimo, sifananishe na jingine,
kwa yote yaliomo, sitataka mwingine
sijitie simanzi, moyo wangu ni wako.

sijitie simanzi, moyo wangu u wako,
mtima una mapenzi, kokote uliko,
njoo kwangu unienzi,maana sitoki kwako,
Kwa sherehe na shangwe, tukuwaambie wazee.

 

Find More Writings by Bee Illustrated here