Chapisho La Siku Ya Mashujaa na Alffie

Kwanza ningependa kumpongeza aliyependekeza kuwa na Jumakiswahili (yaani siku ya kiswahili kama vile Jumamosi ni siku ya kwanza, Jumapili na kadhalika) kwa mtandao wa mawasiliano kwa jina “Twitter”. Ni pendekezo hili lilinifanya niamue kuandika chapisho hili kwa lugha ya taifa ya Kiswahili. Shujaa ni mtu mashuhuri katika jambo; bingwa, shupavu, mshindi, stadi kwa jambo ama mtu ambaye alifanya jambo ambalo linatambulika na watu fulani kama kitendo cha kupewa sifa. Ni kwa sababu hii siku ya Mashujaa imefanywa kuwa siku kuu. Nami leo ningependa kuwatambua baadhi yao na kuwapa heshima wanayostahili.

Ee Mungu nguvu yetu

Ilete baraka kwetu

Haki iwe ngao na mlinzi

Natukae na undugu

Amani na uhuru

Raha tupate na ustawi.

Kwanza, nitaanza na mashujaa ambao walikuwa hai wakati nchi hii yetu ilikuwa inapigania uhuru ambao tunaosherehekea sasa na kuishi, wakati mwingine bila kukumbuka kuwa wakati mmoja hapo kale haukuwa!

Sita Waliofungwa Kapenguria

Dedan Kimathi Waciuri

Kuna wale wajulikanao sana kama Bildad Kaggia, Kungu Karumba, Fred Kubai, Paul Ngei na Achieng’ Oneko ambao waliwekwa gerezani na rais wa kwanza wa Kenya ambaye sitamtaja hapa kwa sababu ametambulika sana. Sura yake iko kwa hela zetu, mwanawe ako serikalini, ana mali (na mashamba!!) kila mahali – nadhani amepata heshima ya kutosha!! Dedan kimathi Waciuri kwa ujasiri wake na kuifia nchi hii. Sitawasahau akina Tom Mboya, MAU MAU na wengine wengi waliopigania uhuru wetu lakini hawajapata kutambulika. ASANTENI!

Amkeni ndugu zetu

Tufanye sote bidii

Nasi tujitoe kwa nguvu

Nchi yetu ya Kenya

Tunayoipenda

Tuwe tayari kuilinda

Evans Wadongo

David Lekuta Rudisha

Ngugi Wa Thiong'o

Evans Wadongo CNN Hero kwa kuchukua jukumu la kufanya mabadiliko mahala aishipo na mahala usaidizi unahitajika bila ya kumtegemea ‘mheshimiwa’ fulani. Ngugi Wa Thiongo kwa kusimama wima akitetea anachokiamini hata baada ya kutiwa gerezani. David Rudisha kwa kutuonyesha kuwa hakuna rekodi ambayo haiwezi kuvunjwa tena na tena! Timu ya raga kwa jina linalofaa la Shujaa pia ni lazima niwataje kwa kuweza kuipa Kenya sifa zinazoenea hadi kona zote za dunia hii!

 

Shujaa

Kimani Muruge

Kimani Maruge kwa kutukumbusha kuwa umri si jambo la kumzuia yeyote yule kufanya kile atakalo kulifanya na ana nia ya kuifanya! Maulana aiweke roho yake mahali pema peponi!

Kwa mashujaa wengine kama Wangari Maathai, John Githongo na wengine wengi tutazidi kuwapa heshima wanazostahili na kuwaunga mkono panapohitajika. Mashujaa wa Kenya ya leo ni wengi lakini nimetaja hao kadhaa tu. ASANTENI! Natujenge taifa letu

Ee, ndio wajibu wetu

Kenya istahili heshima

Tuungane mikono Pamoja kazini

Kila siku tuwe na shukrani Shujaa nitakao wataja sasa ni wewe na mimi yaani Wakenya kwa jumla! Mtu yeyote yule anayejitambua kuwa Mkenya ni shujaa! Mengi tumeyaona na kuyapitia; mengi tumevumilia na kujivunia; mengi tungependa hayangetendeka lakini yalitendeka lakini bado tupo wima. Hata baada ya maovu ya watu fulani, bado tulijitokeza kwa wingi kuipigia kura katiba iliyopendekezwa na hata ingawa kulikuwa na tofauti ya maoni kuihusu katiba hiyo, hapakuwa na uhasama!! Kwa sababu hiyo.. kama wewe ni MKENYA,WEWE NI SHUJAA!! Heko kwako!

Hii ni kazi ya "Dozart Designs" (Alisha Picha)

Hii ni kazi ya “Dozart Designs” (Alisha picha)

Kwa hivyo kama wewe wajivunia kuwa Mkenya..jipongeze na uedelee kujivunia!

Hii ni kazi ya WordTracer(www.twitter.com/Wordtracer) pata picha hii ya kuweka kwa kompyuta yako kwa kuailisha picha (clicking on picture)Find more writings by Alffie here