Nipe nikupe, maneno hayo usemayo,
usinitumie sin’tupe, mimi wako mwenziyo,
sijifananishe kupe, mambo hayo tia moyo,
kwa wakati simo, sijitafutie mwingine.
kwa wakati simo, sijitafutie mwingine,
mapenzi mambo muhimo, sifananishe na jingine,
kwa yote yaliomo, sitataka mwingine
sijitie simanzi, moyo wangu ni wako.
sijitie simanzi, moyo wangu u wako,
mtima una mapenzi, kokote uliko,
njoo kwangu unienzi,maana sitoki kwako,
Kwa sherehe na shangwe, tukuwaambie wazee.
Find More Writings by Bee Illustrated here
dyiembo
/ November 3, 2010Habari ndio hii basi….Watu watalijua jiji raundi hii
Pre7amer
/ November 3, 2010like i said, reading is hard. i only made thru the fist stanza.
lakini Hongera Bee!!! Maandishi yako mufti mno
Bee Illustrated
/ November 4, 2010@Dyiembo na Pre7amer….ahsante kwa kusoma na kutoa maoni yenu.